Watu wengi walijitokeza kwa mapambo mbali mbali kusherehekea siku kuu ya Madaraka huku wengine wakionyesha uzalendo wao katika hafla hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kamera zetu zilifanikiwa kumnasa kijana mmoja katika uwanja wa Gusii, Kaunti ya Kisii akiwa amejipamba kwa ngozi ya ng’ombe, mkuki, ngao, pembe ya ng’ombe kwa kuwonyesha uzalendo wake.

Akiongea na na mwandishi huyu siku ya Jumatatu, mzalendo huyo alidai kuwa Wakisii wamesahau mila zao kwani vifaa waliokuwa wakitumia kitambo katika vita au kuonyesha utamaduni wao havipo tena na kuongeza kuwa ndio maana aliamua kuwa nazo ili kutambua uzalendo wa jamii ya Wakisii.

Aidha, alisema kuwa hajawai kosa sherehe yoyote iwe ya Serikali ya Kaunti au ile ya kitaifa.

“Mimi sijawai kosa kushiriki katika sherehe yoyote inayofanyika katika uwanja huu wa Gusii na siwezi kosa kuja na vifaa hivi vyangu maanake vifaa hivi ndivyo vinaonyesha uzalendo wangu,” alihoji Mzalendo huyo.

Kwa sasa ameiomba sekta inayohusiana na utamaduni kukumbuka vifaa ambavyo jamii ilikuwa inatumia ili hata kizazi kijacho kiwe kinafahamu vifaa hivyo.