Kijana wa umri wa miaka kumi na saba amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshtakiwa, Barrack Ndegwa, alikubali shtaka la kuvunja duka na kuiba zaidi ya shilingi elfu 30, mali ya babake, Ndegwa Marondo.

Mshtakiwa huyo alitekeleza kitendo hicho tarehe 10 mwezi Aprili, katika eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa alipatikana na shilingi elfu kumi, alipotiwa mbaroni na afisa wa upelelezi katika eneo la Likoni.

Hakimu Diana Mochache aliagiza kuletwa kwa cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa huyo kabla ya kutoa hukumu.