Kijana mwenye umri wa makamo amefikishwa katika Mahakama kuu ya Mombasa kujibu mashtaka mawili ya mauaji.

Share news tips with us here at Hivisasa

Adam Mustafa Juma anadaiwa kuhusika katika mauaji ya Mohamed Usi mnamo Februari 6, 2012 katika eneo la Majengo.

Aidha, anakabiliwa na shtaka la pili la kutekeleza mauaji ya Gadaff Mohamed kati ya Januari 4 na 5, 2013 katika eneo la Guraya.

“Sikuhusika katika kutekeleza mauaji hayo. Hizo ni tuhuma tu za kuniharibia jina,” alisema Juma.

Mshtakiwa huyo alikanusha mashtaka yote mawili mbele ya Jaji Dora Chepkwony na kunyimwa kuachiliwa kwa dhamana.

Juma anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kisha kutorokea mafichoni nchini Saudi Arabia kabla ya kutiwa mbaroni.

Kesi hiyo itasikizwa Julai 18, mwaka huu.