Kijana wa umri wa makamo amefungwa miezi mitatu gerezani kwa kosa la kupatikana na kitambulisho bandia.
Mahakama ya Mombasa ilielezwa kuwa Oktoba 2,2015, Victor Kiplangat alikamatwa na polisi na kupatikana na kitambulisho na cheti cha kuzaliwa visivyofanana kimajina.
Kiplangat alikubali makosa hayo siku ya Jumatatu mbele ya hakimu mkuu wa Mombasa Susan Shitub, na kuitaka mahakama imsamehe kwa kutokuwa makini na kubeba kitambulisho cha mjombake baada ya kushughulikia hati ya nyumba.
Hakimu Shitub ilikubali kilio chake na kumpa faini ya shilingi elfu 15 ama kifungo cha miezi miwili gerezani.
Kiplangat yuko na siku 14 za kukata rufaa kupinga uamuzi huo.