Kijana mwenye akili taira amefikishwa kizimbani kwa kosa la kupatikana na kipande cha bangi.
Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa mshtakiwa huyo, Nickson Bao, alipatikana na kipande cha bangi chenye thamani ya shilingi 20 katika eneo la Kibokoni, mnamo Aprili 11, 2016.
Mshukiwa huyo alikubali shtaka hilo siku ya Jumanne mbele ya Hakimu katika mahakama ya Mombasa Irine Ruguru.
Kijana huyo aliambia mahakama kuwa yeye ana akili taira na anahitaji kupata matibabu ya haraka.
Aidha, aliitaka mahakama kumzuilia katika Gereza la Shimo la Tewa ili aweze kupata matibabu.
Kesi hiyo itatajwa mnamo Aprili 26, 2016 ili kijana huyo kupewa nafasi ya kusomewa maelezo ya kesi yake kabla kuhukumiwa.