Kikao cha kuchunguza wizara ya pesa na utajiri wa maafisa wa wizara hiyo katika kaunti ya Kisii kimesimamishwa kwa mda.
Hii ni kufuatia ukosefu wa idadi kamili ya wanakamati ambao wangeendesha kikao hicho mnamo siku ya jumatatu.
Ombi la kuchunguza maafisa hao pamoja na wizara hiyo liliafikiwa na kamati ya bunge la kaunti la Kisii baada ya wanakandarasi kutaka maafisa hao kuchunguzwa.
Akizungumza siku ya Jumatatu, mwenyekiti wa kamati hiyo Koina Onyancha alisema vikao hivyo vilisimamishwa baada ya baadhi ya wanakamati kusafiri katika kaunti ya Meru kuhudhuria kongamano la ugatuzi huku akisema vikao hivyo vitarejelewa baada ya kongamono hilo kukamilika.
“Hatungeendelea na kikao cha leo maana idadi kamili ya wanakamati haikuwa hivyo basi tumeahairisha hadi siku tatu sijazo,” alisema Onyancha.
Wizara ya fedha na maafisa wake wanastahili kuchunguzwa ili kuonyesha uwazi kwa mujibu wa wanakandarasi wa kaunti ya Kisii.