Kikao kilichoandaliwa na wakaazi wa wadi ya Esise Kaunti ya Nyamira kumuuliza maswali mwakilishi wa wadi hiyo Teresa Nyaanga ili kubaini jinsi mwakilishi huyo ametekeleza maendeleo katika wadi hiyo kilizua ugonvi baada ya wafuasi wa mwakilishi huyo kugombana na wakaazi wa eneo hilo na kikao hicho kupelekea kikao hicho kusimama kuendelea.
Wakaazi wa eneo hilo waliandaa kikao hicho siku ya Ijumaa katika eneo la Manga ili mwakilishi huyo kuelezea ni miradi ipi amefanya katika eneo hilo ndiposa wafuasi wake walizua labsha na kupelekea kikao hicho kusimamishwa.
“Tuliandaa kikao na mwakilishi wa eneo hii Teresa Nyaanga ili aeleze jinsi amefanya maendeleo na ni miradi ipi amefanya na kutuelezea kiasi cha pesa kimetumika tangu aingie mamlakani lakini wafuasi wake wamezua labsha na hiyo ni ishara ya kuonyesha mwakilishi hangeweza kuyajibu maswali hayo kuna ufisadi kwa wadi hii,”alihoji Jackson Bosire mkaazi.
Kwa upande wake mwakilishi huyo Teresa Nyaanga alisema kikao hicho kiliandaliwa na maadui wake wa kisiasa ndiposa akashindwa kuelewana na wakaazi hao.
Wakaazi hao wanadai kuwa kuna ufisadi wa pesa katika eneo hilo na kusema sharti wafanyiwe maendeleo kabla hawajaanza kukusanya sahihi za kumwondoa mwakilishi huyo kwa kiti kwa kile wanadai kuwa kuna ufisadi.
Wakati uo huo wakaazi hao walisema mwakilishi huyo hajawai kuwahusisha kwa maendeleo na kusema sharti wahusishwe kwa maendeleo na kujua hali ya maendeleo ilivyo.
“Kuna ufisadi kwa wadi yetu maana wasimamizi wa maendeleo wananunua taa moja katika wadi hii na wanaandika pesa zimetumika ni shillingi millioni 26 tunasema kuna ufuisadi unaendelea katika wadi yetu,”alisema perer Omwanza mkaazi.