Vijana wa eneo Bunge la Bomachoge Borabu Kaunti ya Kisii wamesema kuwa wako tayari kuanzisha miradi mbalimbali ili kujiimarisha kimaisha.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongea na Mwandishi huyu wa Habari siku ya Jumatano asubuhi katika eneo la Menyenya, vijana hao walisema kuwa chama ambacho watakianzisha kitawatembelea wanafunzi katika Shule mbali mbali ili kuwapa motisha ya kusoma na jinsi watajiimarisha kimaisha baada ya masomo yao katika shule ya Upili.

Hii ni baada ya baadhi ya vijana wa umri mdogo katika eneo hilo kujiingiza katika mambo ya ulevi na kuwa na uhusiano wa mapenzi na wanafunzi wenzao shuleni, jambo ambalo linahofiwa kuwa huenda ukachangia kuacha masomo kwa baadhi ya wanafunzi hao.

Aidha vijana hao wakiongozwa na Erick Makana na msaidizi wake James Omete, waliomba viongonzi kutoka eneo hilo kushirikiana nao ili kutimiza ndoto yao katika siku sijazo kama vijana.

“Tunaomba viongonzi wa eneo hili wakiwemo Wawakilishi wa Wadi mbali mbali katika eneo Bunge letu la Bomachoge Borabu, waungane nasi watufadhili kifedha ili tuendeleze na kutimiza ndoto yetu,” alihoji Makana.

Wakati uo huo, vijana hao walikiri kuwa wanahitaji kufanya miradi mbali mbali kama ya maji ili watu wanufaike na mradi huo ambao utawasaidia kupigia umaskini kwaheri katika eneo hilo.

“Mradi wa maji utakuwa wa kwanza ili watu wasiwe wanasumbuka wakitafuta maji, kisha baadaye mradi wa mikopo utafuata ili vijana wa eneo hili wajiimarishe kimaisha,” alisema James Omete mwanachama.