Huku uchaguzi mkuu wa 2017 ukikaribia, kikundi kimoja maarufu kama Kalewa Self Help Group katika wadi ya Kivumbini Nakuru mashariki wameapa kuhubiri amani. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya kupata uhamasisho kutoka kitengo cha haki na amani kinachosimamiwa na muungano wa watawa wa kanisa katoliki. 

Akizungumza siku ya Jumapili, mwenyekiti wa kikundi hicho Abel Odhiambo alipongeza kanisa katoliki kupitia kitengo cha haki na amani kwa kuzidi kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya amani. 

Hata hivyo, ametoa wito kwa vijana kutokubali kutumiwa na wanasiasa na badala yake washirikiane kuhubiri amani. 

Picha: Wanachama wa Kalewa Self Help Group Nakuru. Wameapa kuhubiri amani na kuwahamasisha wakazi wa Nakuru kuwaunga mkono. PMambili/Hivisasa.com