Zaidi ya jamii 400 ya Wahanga waliofurushwa kutoka msitu wa Mau na ambao wangali wanaishi Kambini wanahofia kawamba huenda mwaka mpya utawapata kambini ikiwa Serikali haitachukua hatua ya kuwapa makao.
Kulingana na Mwenye kiti wa Wahanga hao Antony Sang ni kuwa jamii hizo hazina furaha wakati huu wa msimu wa Krismasi kwani wangali wanateseka kambini huku wakikosa hata mahiaji yao ya msingi
''hatujapokea chakula chochote cha msaada kutoka kwa serikali kwa mda mrefu sasa kama ilivyokuwa ada na hali ingale ileile ya uchochole''Sang akasema
Wahanga hawa sasa wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake Ruto kutimiza ahadi yao waliyoitoa kuwa watawapa makao kabla ya mwisho wa mwaka huu huku wakidai kuwa wengi wao wangependa kujiendeleza kimaisha katika mashamba yao.
Baathi ya Kambi ambayo jamii hizo zinaishi ni pamoja na Kurbayat,Kipk,Ongor,Tirigoi,Kusumek ,Chebugen na Kiletien