Wamama wote kutoka kaunti ya Nyamira na ile ya Kisii wameombwa kujiunga pamoja katika vikundi vya maendeleo katika maeneo yao ya bunge ili kujiendelesha kimaisha.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea siku ya Jumapili, mwenyekiti wa chama cha wamama wanaokausha mboga katika eneo bunge la Borabu kaunti ya Nyamira Margret Ombuna alisema huu ndio wakati wamama wanastahili kuwa pamoja na kijiinua kimaisha.

Mama Magret alisema chama chao cha kukausha mboga ambacho kilianza miaka kumi na tano  iliyopita kimekuwa cha msaada mkubwa hasa wakati kunapokuwa na kiangazi na mboga kukosekana.

“Wakati tulishuhudia kiangazi kwa miezi tatu imepita, kwa kweli tumekuwa tukiuza mboga zetu na  zimetusaidia pakubwa,” alisema Ombuna.

Aidha, alisema mboga hizo zilisaidia pakubwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008, wakati tena hapakuwa na mboga.

“Kwa hivyo tunaomba wamama wengine kuiga mfano wetu na kukausha mboga nyingi hili zitusaidie siku sijazo,” aliongeziea Ombuna.

Aliongezea kuwa mboga aina ya managu ni dawa kwa binadamu, hasa wakati mtu ana kidonda.

Chama hicho kimeomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwatengea pesa ili kuendelesha mradi huu.

Pia wameomba gavana John Nyagarama kuwajengea kiwanda cha kukausha mboga hizo katika eneo bunge la Borabu.

“Huwa tunaenda hadi mji wa Kisii ili kukausha mboga zetu ambao huchukua siku tatu kukauka kwa sababu huku ndio kuna vitanda vya kukaushia mboga,” alisema Ombuna.