Gavana wa Kilifi akiwahutubia wafuasi wa ODM siku ya Jumatano muda mchache baada ya Joho kuandikisha taarifa katika makao maakuu ya uchunguzi. Picha: Amason Kingi/ facebook.com

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Kilifi Amason Kingi amepuuzilia mbali tishio la kufunguliwa mashtaka kwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho kufuatia tuhuma za kugushi vyeti vyake vya elimu.Akizungumza siku ya Jumatano muda mchache baada ya Joho kuandikisha taarifa katika makao makuu ya polisi, Kingi aliwahakikishia wafuasi wa ODM kuwa watatetea Joho hadi mwisho."Nimekuja Mombasa leo kama wakili na wala sio kama Gavana wa Kilifi. Tumeenda pale tukaona yale yote ambayo yalikuwa yamewekwa mezani na nataka niwaambie kama wakili kwamba hakuna kesi ya kisheria ilioko bali ni kesi ya kisiasa," alisema Kingi.Vile vile Kingi aliwahimiza wakaazi wa Mombasa kusimama kidete na Joho na kumpigia kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti."Tunataka tuwaambie Jubilee, kesi ya siasa humalizwa jukwaani haipelekwi kotini lakini kwa sababu ni waoga wanataka kutumia vifaa vya nguvu vya serikali kututisha. Wanafikiri eti kumpeleka Gavana Joho katika makao makuu ya uchunguzi watamlemaza. Ni dhana potovu na ukweli ni kwamba wanazidi kumtia makali wenyewe,” alisema Kingi.Aidha, Kingi alimfananisha Joho na mkombozi wa taifa la Afrika Kusini hayati Nelson Mandela kutokana na madhila anayozidi kuyapitia."Gavana Joho leo anaiingia ukumbi tafauti kwani yuko kiwango cha Nelson Mandela. Wakaazi wa Mombasa lazima musimame bega kwa bega na Mandelaa wenu. Mandela alitetewa na vijana kutoka mtaa wa wamabanda, sasa wengi wanaomuuunga mkono ni watu wa tabaka la chini,” alisema Kingi.