Viongozi wa kisiasa eneo la Pwani wamehimizwa kuwa na ushirikiano pamoja na kushinikiza umoja miongoni mwa jamii ili kuzuia kuwagawanywa wakazi katika misingi ya vyama, kisiasa na ukabila.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wakazi katika eneo la Rabai siku ya Jumatatu, Gavana wa kaunti hiyo Amason Jefa Kingi amesema kuwa tatizo kuu la mgawanyiko katika uongozi wa pwani husababishwa na viongozi wenyewe na wala sio wananchi.

“Lazima kwa viongozi tuungane na kuwasaidia wananchi wetu lakini sio kuwalaumu wakazi kwani sisi viongozi wenyewe ndio tumechangia mgawanyiko,” alisema Kingi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa muungano wa wabunge wa Pwani na ambaye pia ni mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga amesema kuwa mikakati mwafaka imeidhinisha kuhakikisha kuwa vijana wanapata ajira.

“Tumepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa tunatembelea makampuni yote na kujadiliana nao ili kuwasaidia vijana wetu kuapata ajira,” alisema Mwingi.

Picha: Gavana wa kaunti ya Mombasa Amason Jefa Kingi akiwaomba wakazi kuungana na viongozi wao ili kuhimarisha maisha.