Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua ameshtumu baadhi ya ripoti kwamba idara ya zima moto imekuwa ikitelekeza majukumu yake visivyo.
Akizungumzia mikasa miwili ya moto iliyotokea mjini humo, Mbugua alisema idara ya zima moto ilijaribu kila iwezelo katika matukio hayo mawili.
"Idara ya zimamoto ilijaribu lakini maji yaliisha na ikalazimu idara hio kuenda kujaza tangi tena," Mbugua alisema.
Wakati huo huo alitoa pole zake kwa wafanyibiashara wa maduka yaliyochomeka ya Rumishi na Nakuru Poly.
Mbugua aliwasuta viongozi ambao kila mara hunyosha kidole cha lawama tatizo linapotokea.
Alikuwa akizungumza katika makao makuu ya kaunti ambapo alitoa wito kwa viongozi kushirikiana.