Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani katika hafla ya awali. Picha/ thecoastcounties.com

Share news tips with us here at Hivisasa

Siasa za kiti cha ubunge cha Lungalunga zinazidi kupamba moto, huku aliyekuwa mwalimu mkuu wa Shule ya upili ya Kinondo, Rasaule Juma Kassim, akitangaza kuwania kiti hicho kupitia tiketi ya Ford Kenya.

Juma analenga kumbandua mamlakani mbunge wa sasa Khatib Mwashetani aliyejiunga na Jubilee.Rusaule amesema kwamba hatua ya Mwashetani kujiunga na Jubilee haijaleta natija yoyote kwa wenyeji wa Lungalunga na kudai kuwa Mwashetani alifuata maslahi yake binafsi.Rusaule amejipigia debe na kusema kwamba yuko katika nafasi bora ya kubadilisha maisha ya wakaazi wa Lungalunga.“Nitashinda kiti hiki cha ubunge na nitahakikisha kuleta maendeleo kwa wananchi,” alisema Rusaule.Aidha, amewataka wananchi kumpigia kura ili kuweza kuwaongoza na kuwaletea maendeleo mashinani.“Nipigieni kura niweze kuwaletea maendeleo mashinani kinyume na anavyofanya Mwashetani,” alisema Rusaule.Zaidi ya wagombea 10 wamejitokeza kuwania kiti hicho.