Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulikuwa na kisanga mjini Naivasha Jumatatu baada ya vijana wanaobeba mizigo ya abiria kwenye kituo cha matatu cha Kinangop mjini humo kumkamata mmoja wao na kumuosha hadharani.

Wasafiri waliokuwa wakielekea maeneo tofauti walipigwa na butwaa huku wakitizama kijana huyo akioshwa, baada ya kususia maji kwa takriban miezi mitatu.

Mmoja wao John Kariuki alisema wamekuwa wakimtaka kijana huyo mwenye umri wa makamo kutilia maanani usafi lakini akatia maskio yake nta, jambo lililowalazimu kumwosha mbele ya umma.

Yasemekana uchafu na uvundo aliokuwa akitoa, ulikuwa ukiwafanya vijana hao ambao ni maarufu miongoni mwa wasafiri kama 'beba',  kunyimwa kazi na wateja wao.