Kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya Mombasa amewasilisha ombi mahakamani la kutaka kesi ya wasichana wanne wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la al-Shabaab kusikizwa katika Mahakama ya Shanzu kwa madai ya usalama.
Ombi hilo liliwasilishwa mbele ya Hakimu Teresia Matheka siku ya Jumanne baada ya hakimu aliyekuwa akisikiza kesi hiyo, Simon Rotich, kujiondoa wiki iliyopita.
Maryam Said Aboud, Ummulkheir Sadri Abdalla, Khadija Abubakar Abdulakadir na Halima Adan walikamatwa tarehe 27 mwezi machi katika eneo la EL Wak huko Mandera.
Mahakama itatoa mwelekeo tarehe 19 mwezi Mei kuhusu iwapo kesi hiyo itasikizwa katika Mahakama ya Shanzu au itaendelea kusikizwa mjini Mombasa.