Kiongozi wa walio wengi kwenye bunge la kaunti ya Nyamira Laban Masira amemtaka gavana wa kaunti hiyo kutowapendelea mawaziri wa serikali yake wasio wajibika kazini. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya Alhamis, Masira alisema sharti mawaziri wanaokisiwa kuvuja pesa za umma wachukuliwe hatua za kisheria. 

"Waziri yeyote yule atakayepatikana na hatia ya kutumia vibaya mali ya umma sharti achukuliwe hatua za kisheria," alisema Masira. 

Masira aidha alisuta madai ya uonevu yanayoibuliwa na baadhi ya mawaziri wanaochunguzwa na kamati uwekezaji na hazina ya pesa za umma kuhusiana na kushiriki ufisadi. 

"Haya madai ya baadhi ya mawaziri kudai kuwa wanaonewa na kamati ya PIAC inayowachunguza kuhusiana na matumizi mabaya ya mamlaka na pia uvujaji wa pesa za umma hayana msingi," aliongezea Masira.