Eneo bunge la Kisauni ndiyo inayoongoza katika usajili wa kura katika kaunti ya Pwani ikiwa imesajili watu 7,122 kama wapiga kura.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na afisa wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka Amina Soudi, viongozi wa eneo bunge hilo wamechangia pakubwa kuandikishwa kwa namba hiyo kwa kuwa waliandaa mafunzo kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uchaguzi.

Soudi ametoa takwimu za eneo bunge la kaunti za Mombasa huku Nyali ikisajili watu 4,451, Likoni 4,745 na kusema kuwa shughuli ya usajili ya wapiga kura itaendelea katika afisi za tume hiyo na kuwataka viongozi kuwahimiza wakaazi wa eneo bunge zao kufika ili kujisajili.