Kamanda wa polisi katika Kaunti ya Nakuru John Mwanga Koki amesema kwamba huenda kitengo cha polisi wa kupambana na ugaidi al maarufu kama Anti-Terror Police Unit (ATPU) kitaanzishwa hivi karibuni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kamanda Koki aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari afisini mwake, alibaini kuwa itakuwa hatua kubwa na muafaka ya kupambana na ugaidi katika eneo hilo.

Aidha Koki alisema kwamba ingawa vituo sawia viko jijini Nairobi pamoja na eldoret, kituo hicho kikianzishwa katika Kaunti ya Nakuru, kitaweza kukabiliana na visa ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika eneo hilo katika siku za hapo awali.

Ili kukabiliana kikamilifu na waalifu, Koki amewaataka wakaazi wa Kaunti ya Nakuru kushirikiana na polisi ili kuhakikisha kuwa hatua hiyo ya kujengwa kwa kituo hicho inafaulu.

Matamshi haya yanajiri huku jitihada za kupiga jeki hali ya usalama zikiendelezwa katika maeneo mengi ya Kaunti hii sawia na kitaifa nzima ya Kenya.