Kitengo spesheli cha polisi kitabuniwa ili kukabili ongezeko la ujambazi ambao imeshuhudiwa jijini Nakuru na viungani mwake.

Share news tips with us here at Hivisasa

Miezi chache iliyopita, Nakuru imeshuhudia mauaji mengi: Mwezi wa Januari wafanyibiashara wawili waliuliwa na viungo vya miili yao kupelekwa hadi chumba cha kuhifahdi maiti ya City mjini Nairobi.

Pia mhadhiri wa chuo kikuu cha Egerton aliuawa na watu wasiojulikana tarehe Febrauari 15.

Kitengo hicho cha polisi kikiongozwa na kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Rashid Barua pamoja na kamanda wa idara ya uchunguzi wa uhalifu watakua na kazi ya kuchunguza na kuwashika majambazi.

Mpango huu wa kubuni kitengo spesheli umeibuka baada ya majambazi wawili kuuawa siku ya alhamisi wiki jana katika eneo la ikulu ya rais kwenye barabara ya Nakuru-Nairobi na jambazi mwingine akapigwa mawe na kundi la watu huko Gilgil Ijumaa jioni.

"Hali imezidi kuwa mbaya na lazima tukabiliane na majambazi hawa bila huruma," alisema Bw Barua.

Mbunge wa Nakuru magharibi Samuel Arama alisema majambazi wamewatia wawekezaji hofu na hivyo ni jambo la busara kukabiliana nao.