Serikali ya kaunti ya Nakuru sasa itatekeleza kazi ya ujenzi wa eneo la kuegesha malori katika kituo cha kibiashara cha Salgaa kilicho kwenye eneo la Rongai katika kaunti ya Nakuru kuanzia wiki ijayo.
Ni thibitisho ambalo limetolewa na naibu gavana wa kaunti ya Nakuru Joseph Ruto aliyezuru eneo hilo Jumatano na kusema kwamba ujenzi huo utaendelezwa na serikali ya kaunti ya Nakuru ingawa eneo hilo la kuegesha malori linafaa kujengwa na serikali ya kitaifa.
Ni mradi ambao amesema utagharimu shilingi milioni 13. 1 ambazo ameweka bayana kwamba tayari zimetengwa na serikali ya kaunti ya Nakuru akiongeza kwamba kando na ujenzi wa eneo hilo la kuegesha magari lenya ukubwa wa ekkari 20, fedha hizo pia zitatumika kugharamia miradi ya ujenzi wa mfumo wa kupitishia maji taka pamoja na ule wa kuweka taa za barabarani.