Huenda huduma katika Kituo cha polisi cha Bamburi zikaimarika zaidi baada ya wahisani kujitokeza na kutoa ufadhili wa kuimarisha kituo hicho kiusalama.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya wahisani pamoja na mfanyabiashara wa Mombasa Ali Mbogo, kukitembelea kituo hicho hapo awali na kushuhudia changamoto ambazo maafisa wa polisi hupitia, hususan katika kunakili kesi za washukiwa wa uhalifu na rekodi zao zingine.

Akiwahushukuru wahisani hao siku ya Jumatano, Afisa mkuu wa Polisi katika kituo hicho Josphat Chebii, amesema kuwa ufadhili wa tarakilishi na vifaa vingine utaboresha zaidi juhudi za maafisa hao kuimarisha usalama.

Aidha, Chebii amewaomba wahisani wengine kuvitembelea vituo vya polisi na kutoa ufadhili wao kuhakikisha kuwa maswala ya usalama katika Kaunti ya Mombasa yanaimarisha.

"Tunawaomba wahisani wengi zaidi kujitokeza na kusaidia kuboresha vituo vyetu vya polisi kwa mahitaji madogo madogo, ili kuhakikisha kuwa maswala ya usalama yanaimarishwa zaidi,” alisema Chebii.