Mbunge wa Njoro Joseph Kiuna ameteta uwepo wa hazina ya ustawi wa maeneobunge CDF akisema fedha hizo zimesaidia kuinua hali ya maendeleo Mashinani.
Kiuna amesema idadi kubwa ya wabunge wako tayari kuifanyia marekebisho sheria ili kuhakikisha hazina hiyo inatumika kuabatana na katiba.
Mp huyo amesema CDF haiadhiri mfumo wa ugatuzi akisema hazina hiyo imefanya mabadiliko makubwa katika maeneo bunge tangu mwaka wa 2003 ilipoanzishwa.
Amesema hazina ya CDF imetumika kuboresha huduma za maji, afya, barabara, elimu, kufadhili masomo kwa wanafunzi kutoka familia maskini ikiwemo miradi mingine ya maendeleo.
Amesema muda wa miezi 12 uliotolewa na mahakama kuifanyia marekebisho sheria utawezesha wabunge kutunga sheria zitakazo okoa hazina hiyo ili iendelee kuinua miradi ya maendeleo katika maeneo bunge.
Baada ya mahakama kuu kutoa maamuzi kwamba hazina hiyo inatumika kinyume cha katiba, agizo hilo limesababisha mdahalo mkubwa huku viongozi wengi pamoja na idadi kubwa ya wananchi wakiitaka hazina hiyo kuwepo baada ya kuoja manufaa yake.
Hivi majuzi Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu, Isaac Lenaola, David Majanja na Mumbi Ngugi ambao wamekuwa wakisikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na Kituo cha Uwajibikaji wa Masuala ya Kijamii (TISA) na Kituo cha Ushinikizaji Democrasia na Utawala Mzuri (CEDGG) walitoa agizo Kufutiliwa mbali kwa CDF wakisema hazina hiyo inatumika kinyume cha katiba.