Viongozi hapa nchini wametakiwa kutojihusisha na semi za chuki ambazo huenda zikaleta migawanyiko hapa nchini kwa misingi ya kidini, kikabila na pia kisiasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wakiongozwa na mbunge wa Njoro Joseph Kiuna waliozungumza na wanahabari Jumatatu walisema kuwa taifa ni kubwa kuliko kiongozi yeyote na lina umuhimu kuliko kiongozi yeyote yule.

"Ningetaka wananchi waangalie matamshi yao na haswaa wanapozungumza na wananchi wakati huu ambapo tunaelekea katika uchaguzi. Msimamo wangu ni kuwa kenya ni muhimu kuliko yoyote Yule," alisema Kiuna.

Kiuna aliongeza kuwa matamshi ya chuki ndiyo yaliyosababisha vifo vya watu wengi baada ya uchaguzi wa 2007, jambo ambalo halifai kuonekana tena katika jamhuri ya kenya.

"Yawe ni maneno ya kujenga lakini yasiwe ni matamshi ya chuki , uhasama na kuleta taharuki," aliongeza Kiuna.