Wanaotumia huduma za shirika la feri katika kivukio cha Likoni huenda wakapata afueni ifikapo mwezi Desemba kufuatia kauli ya katibu mkuu katika idara ya usafiri Irungu Nyakera.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bw. Irungu amesema kuwa ifikapo mwezi Desemba, kivukio cha feri cha Mtongwe huenda kikaanza kutumika tena.

Watumiaji wa kivukio cha Likoni kwa mda wamekuwa wakilalamikia msongamano katika sehemu hiyo hasusan wakati wa asubuhi watu wanapoenda kazini na jionii wakirudi majumbani.

Pia wamekuwa wakilalamikia sehemu za kusuburia feri katika kivukio hicho zimekuwa ndogo kutokana na idadi ya watu kuongezeka.

Shughli za usafiri katika kivukio cha Mtongwe zililazimika kusitishwa mwaka 2012 kutokana na hitilafu za feri ya Mv Mvita na Mv Pwani zilizokuwa zikihudumu katika sehemu hiyo.

Aidha Irungu ameeleza kuwa upanuzi wa sehemu za kuegeshea feri katika kivukio cha Likoni pia unaelekea kukalimika ili kutoa nafasi kwa feri zaidi ya mbili kuegesha kwa wakati mmoja pasi na tashwishi. 

Feri nyengine inatarajiwa kuwasili katika kivikuo hicho ifikapo mwakani, huku feri zote mbili zikitengenezwa na kampuni ya Uturuki.

Kivukio cha feri cha Likoni kinatumiwa na zaidi ya watu 300,000 na magari 6,000 kwa siku na idadi hii inatarajiwa kukuwa kutokana na ongezeko la watu katika eneo la Likoni.