Wakulima katika eneo la Olenguruone kaunti ya Nakuru wamenufaika na kiwanda cha maziwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kiwanda hicho katika eneo la kibiashara la Olenguruone kinatumika kuchukua maziwa kutoka kwa wakulima na kuhifadhi kabla ya kuyatarisha na kuuza katika soko mbali mbali.

Josphene Chemutai alisema tangu kiwanda hicho kuanzishwa wamekuwa wakipata huduma bora na pia malipo.

“Hapa tunaleta maziwa na kila mkulima ana hesabu ya lita ambazo huleta. Hiyo inahakikisha malipo yanafanywa kwa njia inayofaa,” Chemutai alisema.

Aidha wakulima wameshukuru serikali ya kaunti ya Nakuru wakisema kuwa kiwanda hicho kitainua ufugaji wa maziwa kwenye eneo hilo. “Malipo yakiendelea kuwa mazuri na sisi tutazidi kuwekeza katika ukulima wa ng’ombe,” Hillary Ng’eno alisema.