Moto ulioteketeza mali katika kiwanda cha Raiply mjini Eldoret haukujeruhi yeyote.
Moto huo unaosemekana kuanza mwendo wa saa tisa alfajiri inahofiwa kuwa utasambaa kuelekea mahali pa kuegeza magari ambayo hubeba mafuta ya petroli kufuatia upepo mkali unaovuma.
Wasaidizi kutoka kitengo cha Red Cross na wazima moto kutoka kitengo cha jeshi cha KDF tayari wamefika katika eneo la tukio ili kupeana msaada wao.
Askari wa kaunti ya Uasin Gishu wanaendelea kuzima moto ambao tayari ulikua umeshika nyaya za stima.
Wafanyikazi wa kiwanda hicho ambao walikua wamefurika nje ya kiwanda hicho wametumwa kurudi makwao na kamanda wa kaunti ya Uasin Gishu .
Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu wanavuta maji kutoka mto sossiani ili kujaribu kuuzima moto huo.
Wiki mbili zilizopita, kitengo cha kutengenezea godoro ilichomeka kufuatia hitilafu za nguvu za umeme.