Mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta leo amezindua kliniki tamba ambayo amemkabidhi gavana wa kaunti ya Uasin Gishu hii leo Jackson Mandago.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akimkabidhi Gavana huyo katika kaunti hiyo, Kenyatta alisema kwamba kliniki hiyo itawasaidia akina mama waja wazito na watoto wa chini ya umri wa miaka tano.

Aidha aliongeza kuwa ni jukumu la kila mmoja kuokoa maisha na hii itafanikishwa ikiwa kila mwananchi atajitolea.Hii ni kaunti ya ishirini baada ya zingine kumi na tisa kukabidhiwa kliniki hizo.

Gavana Mandago alimwomba mama wa taifa mbio za mwisho wa kipindi hicho kiwe katika kaunti hiyo na kuwa wako tayari kuifadhili kama kaunti.Kliniki hiyo ambayo ilipeanwa na benki ya Afrika inatarajiwa kuanza kazi hii leo na itawafaidi wakaazi wote wa kaunti hiyo.

 Kando na hayo,seneta wa kaunti iyo Bw.Isaack Melly aliomba kutofutuliwa mbali kwa pesa za hazina za maeneo bunge ili iendeleze miradi kama itakayonufaisha wananchi.

Vile vile,mama wa kwanza wa kaunti jirani Baringo aliwasihi watu kutoka “city of champions” kujitokeza kwa wingi ili kushiriki kwa mbio hizo za “Beyond Zero Campaign” ambayo inatarajiwa kufanyika wikendi hii mjini Nairobi.

Hafla hiyo aidha ilihudhuriwa na gavana wa kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet Alex Tolgos pamoja na wake wa magavana kutoka kaunti mbali mbali.