Katibu wa Knut tawi la Kilindini Dan Aloo akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Picha/ tupo.co.ke]
Katibu wa muungano wa walimu (Knut) tawi la Kilindini Dan Aloo ameitaka serikali kufutilia mbali marufuku ya safari za usiku.Aloo alisema kuwa marufuku hiyo inazidi kutatiza usafiri wa wanafunzi.Akizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumapili, Aloo alisema kuwa marufuku hiyo imeathiri sekta ya elimu ikizingatiwa wanafunzi wengi wanaosafiri kuelekea shule za mbali wametatizika kufuatia ukosefu wa magari na kusalia nyumbani.“Wanafunzi wanaoishi nje ya Kaunti ya Mombasa ambao huwa wanasafiri nyakati za usiku wametatizika pakubwa huku wengine wakibaki majumbani,” alisema Aloo.Aidha, Aloo aliongeza kuwa mbali na kuathiri wanafunzi, marufuku hiyo imeathiri uchumi na hata kuongeza gharama za maisha kwa Wakenya wa matabaka ya chini.“Uchumi umedorora, vijana wengi waliokuwa wakifanya kazi kwenye magari hayo sasa wamepoteza ajira na wamerudi mitaani kutekeleza wizi,” alisema Aloo.Katibu huyo alisisitiza kuwa serikali inafaa kubuni njia mbadala ya usafiri itakayowaepusha wanafunzi kutofika shuleni wakiwa wamechelewa.Aloo pia ametoa wito kwa watumizi wote wa barabara kuwa waangalifu ili kuepuka visa vya ajali.Aidha, ameyataka mashirika ya kijamii kuingilia kati swala hilo na kuhakikisha kuwa marufuku hiyo inaondolewa kabla ya kuleta madhara zaidi kwa wananchi.“Naomba mashirika ya kijamii na wenye magari kuelekea mahakamani ili suluhu la kudumu kupatikana kwa haraka,” alisema Aloo.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6