Katibu wa chama cha Knut Kaunti ya Mombasa Dan Aloo akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Picha/ the-star.co.ke]
Chama cha walimu nchini KNUT, kimepinga hatua ya serikali kuanza usambazaji wa vipatakalishi katika shule za binafsi.
Katibu mkuu wa chama hicho Kaunti ya Mombasa Dan Aloo alidai kuwa hatua hiyo imedhihirisha wazi kuwa serikali inapanga kufuja kiwango kikubwa cha fedha.Aloo alisema kuwa hatua hiyo itagharimu serikali kiwango fedha nyingi kwa kuwa shule za binafsi ni nyingi ikilinganishwa na zile za umma.Aloo alisema kuwa ingekuwa bora zaidi endapo serikali itatumia fedha hizo kuboresha viwango vya elimu katika shule za umma ikiwemo kushughulikia swala la upungufu wa walimu katika shule hizo.Haya yanajiri baada ya katibu katika Wizara ya Elimu Belio Kipsang kutangaza kuwa shule za binafsi zitaanza kupokea vipatakilishi hivyo pindi vyuo vya Jomo Kenyatta na Moi vitakapomaliza kuvitengeza.