Kufutia uamuzi wa wizara ya elimu kufutilia mbali baraza la kusimamia mitihani ya kitaifa KNEC, mbunge wa zamani wa Subukia amepongeza uamuzi huo na kutaka IEBC ibanduliwe na kuundwa kwa tume iliyo huru na inayoaminika katika utendakazi wake.
"Napongeza kufutiliwa mbali kwa KNEC na naomba kubanduliwa pia kwa IEBC kutokana na kashfa ya chicken gate. Wakenya wanataka tume iliyo huru na inayoaminika," Koigi alisema.
Muungano wa upinzani CORD ulikua katika mstari wa mbele kutaka kufutiliwa mbali kwa tume hiyo inayoongozwa na Isaac Hassan wakidai kuwa hawana imani nayo.