Wakufunzi wa tamasha la muziki kutoka katika eneo la Nakuru linalojumuisha kaunti nane Jumatano walikusanyika katika Chuo kikuu cha Catholic University of Eastearn Africa (GABA) katika Kaunti ya Uasin Gishu ili kuhudhuria kongamano ambayo iliwaleta wakufunzi wa shule ya chekechea hadi ile ya vyuo pamoja.
Kongamano hilo ilikua ikijumuisha Kaunti nane na idadi ya walioshiriki ilikua zaidi ya wakufunzi mia mbili na hamsini na idadi inatarajiwa kuongezeka na kukamilika siku ya ijumaa.Kaunti zilizoshiriki ni Nakuru, Baringo, Narok, Uasin Gishu, Bomet, Kericho, Nandi, Elgeyo Marakwet na majirani wao Trans Nzoia na Samburu.
Akizungumza na wanahabari mwenye kiti wa tamasha hilo eneo la Nakuru katika kitengo cha shule ya msingi Charles Kurgat alisema kuwa madhumuni ya kongamano hilo ni kuhakikisha kuwa wanawaleta pamoja wanafunzi wote kutoka eneo hilo na kuinua hadhi ya tamasha hiyo.
Aidha, Kurgat aliongeza kuwa shule za sekondari wana idadi kubwa ya wanaoshiriki ikilinganishwa na ile ya msingi kwani wao hupata ufadhili kutoka shule zao. Vile vile, aliongeza kuwa wanakumbwa na changamoto kama vile kukosa fedha za kutosha kutoka kwa kila kaunti husika na wanaiomba serikali za kaunti kuwajibika.
Kando na hayo mwenye kiti wa tamasha hilo katika kitengo cha shule za sekondari K.K Robert alihoji kuwa ni vyema kukuza talanta na wanafunzi wanaoibuka washindi watuzwe kwani kwa sasa tuzo wanazopata ni ndogo mno.