Walimu wakuu nchini wameanza rasmi kongamano litakalo waleta pamoja zaidi ya walimu elfu saba wa shule za upili katika ukumbi wa Wild Waters jijini Mombasa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katika kongamano hilo, serikali kupitia Waziri wa Eimu Fred Matiang’i inatarajiwa kuzungumzia kuhusu mapendekezo ya mabadiliko ya mtaala wa elimu.

Mwenyekiti wa chama cha walimu wakuu wa shule za upili nchini John Awiti ametoa wito wa kupunguzwa kwa idadi ya masomo yanayofunzwa katika shule za upili.

Aidha, ametaka masomo hayo kuzingatia zaidi ujuzi wa wanafunzi walio na vipaji.

Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Wild Waters siku ya Jumapili kwenye matayarisho ya kuanza kwa kongamano hilo la 41, Awiti alisema kupunguzwa kwa idadi hiyo ya masomo kutapunguza mzigo kwa wanafunzi.

“Hali hiyo inasababisha ukosefu wa nidhamu pamoja na matokeo mabaya miongoni mwa wanafunzi,” alisema Awiti.

Aidha, mwenyekiti huyo alisema kuwa wanachunguza sababu ya kuwepo kwa visa vya ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili.

Kongamano hilo la wiki moja linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne.