Muungano wa wanafunzi wa dini ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta walifanya kongamano lililowaleta pamoja wanafuzi wote wa miungano ya Kiislamu katika Kaunti ya Mombasa.
katika mahojiano na mwandishi huyu siku ya Jumamosi jijini Mombasa, mwenyekiti wa muungano huo wa wanafunzi wa dini ya Kiislamu Idriss Yuniss, alisema kuwa zaidi ya sheikh watano watahudhuria kongamano hilo ili kuwaelimisha vijana kuhusu mambo tofauti.
Baadhi ya mafunzo yatakayotolewa ni umuhimu wa elimu katika dini ya Kiislamu, ushauri kuhusu ulimwengu wa kisasa, mavazi nadhifu katika dini ya Kiislamu na mazungumzo baina ya shule na mashirika.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 250.
Kongamano kama hili lilifanywa mwisho waka wa 2012.