Hamisi Hare Karisa (kulia) and Saidi Mwamuye Mwalungo (kushoto) wakiwa mahakamani [Picha- Benson Mwangi ]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama mjini Mombasa imeagiza washukiwa wawili wanaotuhumiwa kumuua mhasibu mmoja wa benki  kuzuiliwa wakati kesi inapoendelea.

Wawili hao Hamisi Karisa na Saida Mwalungo wanatuhumiwa kumuua David Wokabi tarehe kumi na saba mwezi huu eneo la Nyali mjini Mombasa.

Mwendesha mashtaka Erick Masila aliitaka korti kuwazuiliwa washukiwa hao kwa siku tano katika stesheni ya polisi ya Bamburi wakati maafisa wa polisi wakiendelea na uchunguzi wao.

Washukiwa hao walikamatwa eneo la Shanzu na maafisa kutoka katika kitengo cha upelelezi  mjini Mombasa.

Wokabi ambaye alikuwa mhasibu wa benki ya Stanbic tawi la Nyali alikumbana na mauti hayo eneo la Nyali mwendo wa usiku alipokuwa akienda haja ndogo.

Jaji Dorah Chepkwony aliagiza polisi kuwazuilia washukiwa hayo kabla ya kushtakiwa kwa mauaji tarehe thelathini na moja mwezi huu.

Polisi pia iliagiza washukiwa hao kupelekwa katika hospital ya mkoa wa pwani kwa uchunguzi wa kiakili