Aliyekuwa waziri wakati mmoja Henry Kosgey amehakikisha kwamba yuko katika Jubilee na anaunga mkono utawala uliopo.
Akizungumza mjini Nakuru, Kosgey alimhakikishia Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwamba wako pamoja.
“Katika siku za awali nimekuwa nikimweleza Naibu rais kwamba tuko pamoja na naunga mkono serikali ya Jubilee, lakini leo nataka kuwaambia sibadiliki," alisema Kosgey.
Kosgey alisema kuwa ana imani Jubilee itashinda uchaguzi mkuu wa 2017 Kwa kishindo.
"2017 tuchukue uongozi, na 2022 pia tutachukuwa," aliongeza Kosgey.
Wakati huo huo, Kosgey ametangaza kuwani Ugavana Nandi katika uchaguzi mkuu wa 2017.
Mbunge huyo wa zamani wa Tinderet vilevile aliteuliwa na rais hivi karibuni kuwa mwenyekiti wa fedha za utalii.