Wakili wa halmashauri hiyo Billy Kongore ameimbia mahakama kuwa KPA wanafanya majadiliano na wamiliki wa mabohari hayo ili kesi hiyo kusikilizwa na kuamuliwa nje ya mahakama. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Jaji Emukule amekubali ombi hilo na kuagiza kutofika mahakamani kwa mkurugenzi huyo. 

Hatua hii inajiri baada ya mahakama kuu kumtaka Catherine kufika mahakamani ili kuweka wazi kwanini alikiuka agizo la mahakama kwa kusimamisha shughuli za mabohari yanayomilikiwa na familia ya gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho, licha ya mahakama kuagiza kutofungwa kwa mabohari hayo. 

Mabohari ya Portside na Autoports CFSs yalifungwa baada ya kuhusishwa na kuendeleza biashara magendo. Kesi hiyo itatajwa tena Julai 11 mwaka huu.