Bi Catherine Wairi ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa Halmashauri ya Bandari nchini KPA.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wairi atachukua nafasi iliyochwa na Gicheru Ndua baada ya kupigwa kalamu mwezi Februari.

Uteuzi huo ulifanywa na bodi ya wakurugenzi wa Bandari chini ya uongozi wa mwenyekiti wa Bandari Marsden Madoka, kabla ya kuidhinishwa na Waziri wa Uchukuzi Bw James Macharia.

Bi Wairi amehudumu katika Bandari ya Mombasa kwa zaidi ya miaka 20, katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kaimu mkurugenzi mkuu na pia mkurugenzi katika kitengo cha uhasibu.

Bi Wairi aliwapiku wapinzani wake wakuu Joseph Atonga na Stanley Chai waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia baada ya mahojiano yaliyofanyika kati yao na bodi hiyo.

Kwa mujibu wa Madoka, Bi Wairi alipata asilimia 72.5 huku Bw Atonga na mgombea mwenza Stanely Chai wakipata asilimia 68 na 58 mtawalia.

Uteuzi huo haujazua mjadala kutoka kwa viongozi wa kisiasa katika ukanda wa Pwani, hasa baada ya shinikizo kutoka kwao wakitaka nafasi hiyo kupewa mtu mwenye asili ya Pwani.

Wakaazi wa Pwani wamekuwa wakilalamikia nafasi chache za ajira katika Bandari ya Mombasa, huku wakisea kuwa wanastahiki kupewa nafasi zaidi.