Halmashauri ya utozaji ushuru nchini KRA, imesimamisha kampuni 21 za mizigo na usafiri zinazohudumu katika Bandari ya Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hatua hiyo inajiri huku KRA ikianza uchunguzi dhidi ya kampuni zinazokwepa kulipa ushuru bandarini humo.

Kamishna wa KRA John Njiraini amesema kuwa halmashauri hiyo imeanza uchunguzi kubaini jinsi vyombo 104 vyenye thamani ya shilingi milioni 100 viliondolewa bandarini kati ya mwezi Juni na Julai 2016, bila malipo ya kodi.

Uchunguzi huo unaelekezwa kwa waagizaji, mawakala wao, watoa huduma ya usafiri, Halmashauri ya Bandari nchini (KPA) na wafanyakazi wanaoshiriki katika shughuli za kutoa mizigo.

Miongoni mwa Kampuni zilizosimamishwa ni:

Siginon Freight Limited, Sim Net Marketing Services, Ataco Freight Services, Mwatec Enterprises Limited, Tiba Freight Forwarders, Logistic Solutions Limited, Reliable Freight Services, Kenya Road Transporters, Bahari Forwarders Limited, Best Crystal Agencies, Route Cruiser Logistics, Skyman Freighters Limited, Wima, Subukia Holdings (K) Limited, Hasmad Cargo Limited, Kenya Tradex Company, Doha Transport and Trading Co Limited.