Serikali ya Kenya imeshikilia msimamo wake wa kuifunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa Kenya.
Kambi ya Daadab ndio kambi kubwa zaidi duniani, na ilianzishwa mwaka 1991 na kufikia sasa inakisiwa kuwa na wakimbizi zaidi ya 500, 000.
Baadhi yao wameishi katika kambi hiyo kwa zaidi ya miaka 20, baada ya kutoroka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia.
Hata hivyo, Kenya imelazimika kuchukua hatua ya kuifunga kambi hiyo baada ya habari za kijasusi kuarifu kuwa wanamgambo wa al-Shabaab hutumia kambi hiyo kupanga mashambulizi ya kigaidi humu nchini.
Kenya ni miongoni mwa nchi zinazoathirika kutokana na mashumbilio ya kigaidi katika kanda ya Afrika mashariki na kati, kiasi cha kupelekea kukosa miradi mikubwa katika kanda hii, ikiwemo mradi wa bomba la mafuta ulioafakiwa kupitia Tanzania badala ya Kenya kama ilivyotajiwa hapo awali.
Rais wa Somalia Hassan Mahmoud alizuru ikulu ya rais jijini Nairobi na kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne na Jumatano, kuhusu swala hilo tata.
Mchakato wa kuwarudisha wakimbizi nyumbani kwa hiari uliafikiwa katika makubaliano kati ya shirika la kuwahudumia wakimbizi la umoja wa mataifa, serikali ya Kenya pamoja na ile ya Somalia.
Hatua hiyo ilishinikizwa baada ya Kenya kushuhudia msururu wa mashumbulizi ya kigaidi huku raia wasiokuwa na hatia wakipoteza maisha katika maeneo mbalimbali.
Shirika la Amnesty lenye makao yake Uiengereza na shiriika la Human Rights Watch lenye makao yake inchini Marekani yamepiinga hatua ya kufunga kambi hiyo, kwa madai kuwa hakuna ushahidi wowote wa wakimbizi wanaoshi katika kambi hiyo kuhusika katika ugaidi.
Licha ya mashirika haya ya haki za kibinadamu yasiokuwa ya kiserikali kukemea na shutumu vikali hatua hiyo, Kenya bado imeshikilia msimamo wake wakufunga kambi hiyo.
Swali ni je, endapo kambi ya Dadaab itafungwa italeta nafuu kwa nchi ya Kenya au italeta majuto?
Sekta ya utalii inayochangia kiwango kikubwa cha uchumi nchini itarudi katika kiwango chake cha zamani na je wawekezaji kutoka nchi za kigeni wataongezeka na kuboresha ubora wa biashara?