Mwakilishi wa wadi ya Magenche eneo bunge la Bomachoge Borabu kaunti ya Kisii Timothy Ogugu amesema usalama utaimarika zaidi nchini ikiwa serikali kuu itatimiza azimio lake la kufunga kambi za wakimbizi katika eneo la Daadab.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mjini Kisii Ogugu alipongeza serikali ya kitaifa kwa kuahidi kufunga kambi za wakimbizi nchini na kusema hilo litaimarisha zaidi usalama nchini.

“Taifa letu la Kenya litakuwa na usalama zaidi ikiwa kambi hizo za wakimbizi zitafungwa maana huenda kambi hizo zikatumika na washukiwa wa ugaidi kutekeleza mashambulizi nchini,” alisema Timothy Ogugu.

Ikumbukwe kuwa serikali kuu ilisema ifikapo mwezi wa 11 mwaka huu kambi hizo za wakimbizi zitakuwa zimefungwa na kusafirisha wakimbizi hao kwenye taifa lao la Somalia kwani wakimbizi hao wamekaa nchini kwa zaidi ya miaka 25 jambo ambalo linadaiwa kugharamisha taifa la Kenya pakubwa.