Shirika la Reachout Centre Trust linaloshughulikia tatizo la dawa za kulevya limesema kufungwa kwa waathiriwa wa mihadharati sio suluhu la janga hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo katika eneo la Pwani Taib Abdrahman, amesema kuwa dawa za kulevya ni changamoto ya kijamii na kuwafunga waathiriwa sio njia moja ya kutatua swala hilo.

Akizungumza na wanahabari katika hoteli moja huko Diani, Kaunti ya kwale, baada ya warsha ya kuwaelimisha polisi kuhusu kukabiliana na waathiriwa wa dawa za kulevya na jinsi wanaweza kuwanasua, Abdrahman alisema suluhu ni jamii kuungana ili kulikabili janga hili kwa kutoa mafunzo yatakayohamasisha jamii kuhusiana na madhara ya utumiza wa dawa hizo.

Itakumbukwa kuwa hivi majuzi Mshirikishi mkuu wa usalama katika ukanda wa Pwani Nelson Marwa alisema kuwa walanguzi wa dawa za kulevya wamebuni njia nyengine za kuingiza dawa hizo nchini na kusema kuwa chuma chao ki motoni.

Alisema kuwa baadhi ya njia zinazotumika na walanguzi hao ni kuungana na wafanyibiashara ambao wanaingiza magari mapya humu nchini, ili kuficha dawa hizo katika baadhi ya sehemu za gari hizo.