Wakaazi wa eneo la Sasimwa katika kuanti ya Nakuru wanalaumu kuondolewa kwa maafisa wa polisi kutoka eneo hilo kama sababu ya kuongezeka kwa utovu wa usalama.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wanasema askari waliokuwa wanaishi katika shule ya msingi ya Sasimwa walioletwa katika sehemu hiyo baada ya kuzuka Kwa vita vya kikabila vya mwaka 2007 wamekuwa wakileta usalama.

Wakaazi walisema maafisa hao wa polisi waliondolewa kutoka eneo hilo mwezi mmoja uliopita.

"Hii serikali sijui inatakaje, mbona maafisa hao waliondolewa na tangu watolewe visa vya wizi vinazidi kuongezeka," mkaazi mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina alisema.

Wakaazi hao walisema kwa sasa wizi wa mifugo umeongezeka sana.

Kwa sasa wakazi hao wanataka polisi hao warejeshwe ili kuimarisha usalama.