Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar amesema kuwa kutamatishwa kwa kesi dhidi ya naibu wa rais na mwanahabari Joshua Sang katika mahakama ya jinai ya ICC ni jambo la busara sana kwa kuwa itapunguza joto la kisiasa nchini.
Akihutubia kongamano la mahasibu katika hoteli moja mjini Mombasa siku ya Jumatano, Omar amesema kuwa kuendelezwa kwa kesi hizo kungesababisha uhasama wa kikabili haswa ikizingatiwa kuwa ucahguzi mkuu wa mwaka wa 2017 inakaribia kufanywa.
Hata hivyo seneta huyo ametoa wito kwa serikali kutumia taasisi za humu nchini kuhakikisha kuwa waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 na 2008 wamepata haki.
Omar amesema kuwa kwa vile mahakama ya ICC Ilitoa uamuzi kuwa ghasia hizo hazikupangwa bali ni watu binafsi walizisababisha basi ni vyema ikiwa watu hao watachukuliwa hatua.