Amekuwa katika vichwa vya habari kwa muda sasa akiwa mwaniaji was urais kwa mara kadhaa kuliko yeyote. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Raila Amollo Odinga ameonyesha hamu yake ya kuwa rais kwa kujitosa mara tatu katika shindano la kufika Ikulu bila kufanikiwa. Je, kosa la kushindwa ni lipi?

Raila ni mmoja was viongozi wanaotumia kujiamini kwao kujitafutia umaarufu kisiasa, na hivyo kudhani watapata viti wanavyovitaka kwa urahisi. 

Katika tuko la hivi punde, alionekana katika kituo kimoja cha Ufaransa akikemea mahakama kuu ya ulimwengu kuhusu kutupiliwa mbali kwa kesi za rais Uhuru na naibu wake William Ruto. 

Hilo lilitimia saa chache baada ya Raila kumpongeza Ruto kuhusu kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo, jamboambalo lilifanya wengi kumuasi kisiasa kutoka Bonde la Ufa na eneo la Mlima Kenya. 

Mbali na hilo, baada ya mwanahabari Waweru Mburu kumkosoa katika makala yake ya Yaliyotendeka, mmoja wa makatibu wake alimwita mkabila kwa kuita msimamo wake uliojaa 'Ukikuyu'. 

Hili pia huenda likaathiri azma yake ya kuwa rais. Wasaidizi wake, wendani na walio karibu naye huenda wakaitupilia mbali na kuifuta azma yake ya kuwa rais mwaka ujao katika uchaguzi mkuu.