Je, wajua kwanini Wakenya wengi huhama usiku?

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Watu huhama usiku kutokana na sababu tofauti. Sio jambo la kushangaza kuona hata matajiri wakisafirisha vitu vyao kutoka pembe moja ya nchi hadi nyingine usiku.

Baada ya kufanya utafiti kwa muda wa miezi kadhaa, nimeweza kutambua baadhi ya sababu zinazowafanya Wakenya wengi kutohama mchana.

Malazi machafu

Asilimia kubwa ya Wakenya hutumia malazi machafu. Kusafirisha malazi machafu ni jambo la aibu. Wapangaji wanaomiliki malazi yasiyovutia huamua kusafirisha vitu wanavyomiliki giza tu linapoingia.

Madeni

Watu wenye madeni huamua kahama usiku ili wasije wakafumaniwa na wanaowadai. Wengi wao huhakisha hukuna yeyote anayejua wanakohamia.

Kukwepa kodi

Kiwango cha juu cha maisha, ukosefu wa kazi na sababu nyinginezo zimefanya Wakenya wengi kutoweza kulipa kodi. Hii ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wapangaji wengi waamue kuhama usiku ili wasilipe kodi. Wapangaji hawa huhakikisha hakuna yeyote anafahamu njama yao ya kuhama ili habari isiwafikie wanaomiliki nyumba.

Kutoroka marafiki, majirani na jamaa

Idadi kubwa ya watu wanaohama usiku huwa hawataki marafiki, majirani na jamaa zao wafahamu walikohamia.

Kuhepa wapenzi

Wanaume kwa wanawake huhama saa za usiku ili wapenzi wao wasifahamu walikotorokea. Kulingana na utafiti wangu, kuna kiwango kikubwa cha watu ambao huhama usiku kama njia mojawapo ya kuhepa majukumu yao kwa familia. Hili swala ni la kawaida kwa wapenzi ambao wamechumbiana kwa muda mchache na kupata watoto bila kutarajia.