Idara ya kuhifadhi wanyama pori nchini KWS imeitaja Bandari ya Mombasa kama mojawapo ya sehemu ambazo biashara isiyohalali ya kusafirisha pombe za ndovu hutekelezwa humu nchini.
Afisa mkuu wa idara hiyo Kitili Mbathi amesema kuwa aidha bandari ya Mombasa hutumika katika kusafirisha pembe hizo nje ya nchi au kuleta kutoka nchi za nje bidhaa zilizotengenezwa na pembe ya ndovu.
Kwa sasa idara hiyo imetoa taarifa kwa idara ya polisi ikitaka uchunguzi kufanyika dhidi ya maafisa bandarini wanaofanikisha biashara hiyo abayo ni haramu humu nchini.
Mbathi alikuwa akizungumza siku ya Jumamosi katika bandari ya Mombasa baada ya maafisa kutoka idara hiyo kufumania shehena kadhaa zilizokuwa na pembe za ndovu.