Vikundi vinavyokopa mikopo kutoka mashirika mbalimbali katika kaunti ya Kisii vimeshauriwa kurudisha mikopo hiyo kwa mda ufahao kuzuia kunyimwa mikopo kutokana na kuchelewa kulipa.
Akiongea mjini Kisii afisa anayesimamia vyama vya mikopo katika kaunti hiyo Vincent Kenyariri alisema ni vibaya sana wakati wanachama wanazuiliwa kukopa mikopo baada ya kuratibishwa na Shirika la Kudhibiti Mikopo (CRB) ambapo mtu anapochelewa kulipa mkopo kwa wakati aliopewa huzuiliwa kukopa pesa kote nchini.
Kenyariri alihimiza wanachama kujaribu kurudisha mikopo kwa wakati unaofaa kuzuia changamoto kama hizo.
“Si vizuri kuzuiliwa kukopa kutokana na ukosefu wa kurudisha mikopo kwa wakati unaofaa, kila mwanachama awe mwangalifu ili tusonge mbele pamoja kwa kupata mikopo na kufanya biashara ili kujinufaisha kimaisha,” aliongeza Kenyariri.