Rais wa LSK Isaac Okero katika hafla ya awali. Amesema mawakili walioteuliwa wana uwezo wa kuusuluhisha mgomo huo wa madaktari. Picha/ the-star.co.ke

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Chama cha Mawakili nchini LSK, kimeteuwa mawakili wawili watakaoongoza majadiliano kati ya serikali na madaktari kuhusu mgomo ulioingia siku yake ya sabini na tano.

Rais wa chama hicho Isaac Okero alisema kuwa wamewateua John Morris Ohaga na Njeri Muriuki, huku Ohaga akiteuliwa kama mwenyekiti wa kamati hiyo ya pamoja itakayoongoza majadiliano hayo.Mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya utetezi wa haki za kibinadamu Bi Kagwiria Mbogori aliteuliwa kama naibu mwenyekiti wa kamati hiyo.Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi, Okero alisema mawakili hao wana uwezo wa kuusuluhisha mgomo huo wa madaktari kwani watatoa muongozo unaofaa baada ya kuangalia pande zote mbili.Okero aidha aliwashukuru mawakili Geoffrey Orao Obura na Micheal Muchemi walioongozwa na Seneta wa Siaya James Orengo kuhakikisha kwamba viongozi wa madaktari waliokua wametiwa mbaroni wameachiliwa huru ili mazungumzo yaendelee.

Pande zote mbili, za serikali na madaktari, zinapaswa kufika mahakamani Februari 23, ili kueleza kuhusu mafanikio yao katika kuusitisha mgomo huo ambao umedumu kwa kipindi cha miezi miwili na nusu sasa.